Siku
hizi zakaribuni mvua imekua ikinyesha kwa wingi na hali yahewa ni
baridi kwa baadhi ya mikoa hapa nchini.Watu hukabiliana na baridi hiyo
kwa njia na namna mbalimbali.Hapa jikoni tunakabiliana na baridi kwa
kikombe cha Maji vuguvugu yenye Tangawizi,mdalasini na asali.
Tangawizi na mdalasini vinasifa yakuleta joto mwilini kwa haraka na pia huongeza uwezo wa mwili kumeng’enya na kutumia chakula (Metabolism).Sifa hizi hufanya viungo hivi kua moja ya viungo muhimu katika kuiweka afya yako salama.Unaweza tumia viungo hivi hata katika mapishi mengine
Mahitaji
- Maji yamoto kikombe 1
- Tangawizi kijiko 1 cha chai (inaweza kua yaunga,au sugua tangawizi mbichi kisha kamua maji yake)
- Mdalasini ½ kijiko chai ( wa unga/uliosagwa)
- Asali Mbichi kijiko 1 cha chai
1.Chemsha maji adi yatokote
2.Katika kikombe weka Tangawizi na mdalasini,kisha mimina maji yamoto.Koroga ili kuchanganya.Funika kikombe kwa dakika tano
- Funika kikombe ili kutunza virutubisho na kutunza joto ili liwezeshe uvunaji wa virutubisho kwenye viungo
- Usichemshe viungo jikoni kwani kufanya hivyo kutapoteza virutubisho na nguvu ya viungo
- Asali huongezwa baada ya joto la maji kupungua ili kuepuka kuuwa enzymes walio kwenye asali,pamoja na kutunza virutubisho vilivyo kwenye asali
- Chuja kabla yakunywa ukipenda
Tafiti za Tiba lishe na
virutubisho zinaonyesha kwamba ni lazima kutumia tangawizi kijiko kimoja
cha chai Wakati wowote unapotumia tangawizi kama tiba lishe ili kupata
matokeo
Naamini kinywaji hiki kitakufaa sana siku za baridi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni